Thursday, February 28, 2013

LIL WYNE NAYE NA YAKE!!!

Msanii maarufu nchini Marekani kutoka kundi la Young Money, Lil Wyne, ametoa taarifa kuwa anmpango wa kujenga club kwaajili ya mashabiki na wapenzi wote wa kundi zima laa YM ili kuweza kufanikishampango mzima wa kuwapa mashabiki burudani wanzostahili.
Taarifazaidi kuhusu sehemu inapojengwa ckub hiyo, na gharama kamili ya ujenzi, vitawekwa wazi hivi karibuni. kaa tayari kupata zaidi kupitia hapa,
 THE SOURCE, MPANGO MZIMA.

BRAND NEW! RIGHT THERE by Justin Beiber

Justine Beiber, ametoa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Right Here,aliomshirikisha msanii Drake.

wasanii wa Kenya watoa Wimbo mpya kuhamasisha mabadiliko katika uchaguzi ujao.Tazama video yake hapa.

Ikiwa ni muda mfupi wananchi wa Kenya kufanya uchaguzi wa viongozi wao, baadhi ya wasanii wameungana kutoa wumbo wa pamoja, unahamasisha Mabadiliko.
Wimbo huo unaokwenda kwa jina la CHANGE umefanywa na wasanii; Avril, Ala C,Rabit,Jua Cali, Sana Ipei, Tande na Jimvati.

Wednesday, February 27, 2013

2030 by ROMA, LYRICS hizi hapa,






[Rhymes Of Magical Attraction], ngoma ikifahamika kama 2030 akiwa na Story.
ARTISTS:        Roma Mkatoliki ft. Story
TRACK NAME:  2030

Tanzania eeehhh (Tongwe Records Baby)
nchi yangu ooohhhh...
VERSE 1:

huwezi kuijenga roma haikujengwa kwa siku moja
iwe kwa raha leo au simba mtoto tanga watakuja
hata pacho pia ni mwamba ila bado anakata viuno
kaskazini bila tanga ni msondo bila gurumo

alisema juu ya mwamba atalijenga kanisa
na halitatikisika waumini tuianze misa
kwenye njaa kula kuku aliyechinjwa na padre hewallah
adhana ikilia amka ukamuombe allah!!

bwaa sheikh mrudie Mungu masanja kawa mchungaji
sujudu mecca madina tajiri hataki kuhiji
maulid ubungo kibangu ndo mishahara ya madrasa
ona rafiki wa padre kawa muhasibu wa kanisa

tenda wanapeana kindugu mwanangu kua uyaone
familia ilikata ringi na mama alibaki mjane
sikuwa na damu ya kiarabu kwamba nitayarithi mabasi
dingi hakutupa msingi ona gari twaifanya taxi

tazama gongo la mboto mtoto kamzaa mtoto
na atalelewa na nani baba ake mmemfunga keko
wape buku waue winga wale watoto wa morocco
mungu atazidi kukulinda kesho utaiona sabato

mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani
ana wake wa3 je watoto watarithi nini?
ndo chanzo cha kurogana na ku2piana majini
huyu akimpandisha makata yule maimuna subian

maana pesa ndo ilifanya tusiwe na tanga ndugu
pesa ilileta ubaguzi kati ya loyola na pugu
pesa ndo ilichochea beef ya nice na dudu
na pesa ndo ilimaliza vita ya ruge na sugu
KIITIKIO
Tanzania eeehhh
mwanangu kua uyaonee
boss acha kisirani gonga muhuri tuwahiii
Nchi yangu ooohhh
mwanangu kua uyaone
Traffic hasira za mkeo barabarani hazifai
Tanzania eeehhh
mwanangu kua uyaone
wanahonga mashabiki ngoma zao wazi-request
Nchi yangu ooohhh
mwanangu kua uyaone
Udini wa ma-presenter wapagani unatucost
VERSE 2:
Aminini nawaambieni ujana ni maji ya moto
mtoto humzika mama leo mama anamzika mtoto
ndo maana mama alisema nisimchumbie mmachame
muraa shusha mapanga naileta posa tarime
leo bahari imechafuka mpemba haishemu karafuu
hatari kama nungwi nahodha sio kirikuu
yakhee nirushie mtumbwi mie mwamba sio kichuguu
hii ni vita ya msambaa mbondei usitie maguu
ona kipindi cha bunge dodoma inanuka ngono
spika akiahirisha bunge wengi watau-support mgomo
wabunge mnadai posho muhonge dada zetu
kuna wanafunzi wa mama salma vyuoni usicheze peku
wazanzibari hawaioni thamani ya huu muungano
ila kulichoma kanisa sio njia ya kuvunja agano
sioni sababu ya ubaguzi na kuua wasio na hatia
wakati aliochanganya mchanga mchanga umeshamfukia
muislamu gani unahonga bongo movie mamilioni
mama anakufa mwaisela kakosa dripu ya quinine
ni heri ujenge msikiti tuitukuze mitume
anasa za bakulutu unatunza wacheza sebene
unamuheshimu ramadhani unazini mbele ya shaban
kama ilishushwa quran twendeni misikitini
anaedhihaki msahafu pengine kanisa halijui
so kulichoma kanisa ni kuuza bible dubai
usihofu kumpoteza mmoja ili kumi waishi vema
watanzania tuna uoga sio amani mnadanganywa
sacrifice for your son and daughter amka kifikra
damu yako iwe chachu ya ukombozi dokta ulimboka
mkinga usimuue mama ili uongeze kipato
utajiri upo kaburini watu wamekufa na ndoto
leo ridhiwani haufanani na makongoro
dah!! sina hela ya kiroba rashidi nigongee ugoro
suka kaiangusha lori ya mafuta yote magendo
waziri anaziuza pembe za ndovu na meno ya tembo
nchi imejaa misitu tuna uhaba wa madawati
tunakula vitu feki TBS mko wapiii
RPC usitume kikosi ili uishushe chadema
italipwa damu ya mwangosi iringa semeni amina
okoa wagonjwa wa saratani mpakani zuia wakimbizi
kuliko kumwaga pesa kwenye tume za uchunguzi
Muhimbili naumwa goti eti dokta kapasua kichwa
mbeya wanapigwa nyundo ili raia wauze mabucha
amana wanatelekeza watoto wanalia
mwananyamala wanatuua na hawaendi jela
Jela anakwenda Kajala
KIITIKIO
Tanzania eeehhh
mwanangu kua uyaonee
boss acha kisirani gonga muhuri tuwahiii
Nchi yangu ooohhh
mwanangu kua uyaone
Traffic hasira za mkeo barabarani hazifai
Tanzania eeehhh
mwanangu kua uyaone
wanahonga mashabiki ngoma zao wazi-request
Nchi yangu ooohhh
mwanangu kua uyaone
Udini wa ma-presenter wapagani unatucost
VERSE 3.

sauti hii itasikika mpaka oldonyo lengai
nikifa naomba nizikwe tanga na mje kwa shambalai
u can kill me bro but u wont kill what am standing for
usiutamani urithi wa baba ikimshuka cd4

eti tuzo sikustahili haa haaa hii ni hatari
tuzo ina chapa ya nani ya kaisari mpe kaisari
hii sio masaki ni ngaramtoni mama anaiuza dadii
muziki umejaa stress kila nyumba ina msanii..(woyoooo!!!)

yanga wamemfukia mbuzi golini simba ana bundi
viongozi wanataka umate umate hawaujali ushindi
utawasikia chuji kachuja kiburi choma mahindi
kapigwa ligi ya jogoo shahidi kamati ya ufundi

vijijini 2po wengi mleteni daktari bingwa
ana ngoma utasikia kalogwa twende kwa mganga
pesa za kujikimu ndo ulichongesha kitanda
kulea mimba sio mchezo ba kijacho haujajipanga

profesa kanyimwa penzi utasikia carol kadisco
carol analea ndugu kwa pesa ya bodi ya mikopo
poleni mnaotafuta C mwaka wa 4 mna risiti
huku headmaster kaenda mjini eti shule imeishiwa chaki

msiwaue wachimbaji wadogo geita inalia
kaburu umempa migodi udsm tuna engineers
unapewa contena la condoms uionge dhahabu
mv spice ilipozama tv inaonyesha taarabu

kamanga hawaiweki lami ili 2vukie busisi
dereva usinitoe kafara ili utimize hesabu ya boss
sina cha kuweka rehani kwenye asasi za mikopo
bajeti ya kilimo kwanza mkulima silioni soko

tanga mmekosa nini amkeni acheni umwinyi
hawa wachaga hawatuwezi ona manka bara 20
bandari chanu relwe chali makamba iinue katani
zito akiroga kasulu si tunamrogea pangani

uchafu wa mrisho unafanya msafi aonekane benja
msisadiki magazeti waandishi wengi kanjanja
vijana ndo nguvu kazi ila wengi wamejaa lutindi
mitaani wamekata ringi hadi figo wanaziweka bondi

majibu ya postmotam ameshayanunua wakili
na hakimu kapewa kiwanja kimara apige kufuli
cheki dola wanainunua kesi napewa kapuku
nawa mpole kama ngamia mbele ya hakimu wa kisutu

RUDIA KIITIKIO





Jan B ft Emmie Playa Haters Brand NEW IN HERE

HUO NI WIMBO WA PILI WA JAMAA BAADA YA KUDONDOKA NA PRETTY GIRL

Tuesday, February 26, 2013

hii ndiyo safari ya mwisho ya Goldie Harvey







Goldie Harvey, amefariki tarehe alhamisi tarehe 14 baada ya kupata maumivu ya kichwa mara tu,mara tu alipotoka Los Angeles nchini Marekani. Harvey amezikwa jana kwenye makaburi ya Vaults and Gardens ambayo ni ya ndugu wa karibu wa familia ya marehemu, huko Ikoyi Nigeria.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen. 

Hivi ndivyo ilivyokuwa London, Dimpoz na Ally Kiba






Timbulo nguvuni Nchini Rwanda

Msanii wa kizazi kipya,maarufu kwa jina la Timbulo anayefahamika kwa vibao vyake kama Domo Langu, Waleo Wakesho,Samsoni na Delila,anashukiwa kukamatwa na madawa ya kulevya jijini Bujumbura nchini Rwanda.
Timbulo alikuwa nchini humo akifanya shows. hata hivyo,habari zaidi kuhusu tukio hilo zinaendelea kufuatiliwa.

Sunday, February 24, 2013

linnah na Amini ndani ya Bagamoyo





amini








linnah
kati ya nyimbo zilizoweza kurindima vilivyo katika ulimwengu wa burudani kwa siku za hivi karibuni,ni wimbo wa Mtima wangu, wa Amini na Linnah. Wimbo huo ambao ulianza kusikika katika vituo mbalambali vya redio nchini kwa miezi mitatu sasa,Video yake iko mbioni kuwa hewani baada ya kuripotiwa kuwa hivi sasa Amini na Linnah,wako Mjini Bagamoyo, kutengeneza video hiyo.
Kaa tayari kuipata video hiyo kupitia hapa.


msanii Prezzo alishiriki mazishi ya Goldie Harvey

Pamoja na mume wa marehemu Goldie Harvey kumuonya vikali hivi karibuni msanii Prezzo kuwa mbali na familia ya Marehemu,Prezzo alihakikisha kwamba anashiriki ibada ya mazishi ya Goldie Harvey nchini Nigeria.

       
       pichani ni rapper Prezzo akiwa na familia ya Goldie Harvey



Kwa sasa rapper Prezzo yupo nchini Kenya.

Saturday, February 23, 2013

Afande Sele mbioni kutoa Albam mpya.

Rapper maarufu nchini Tanzania Afande Sele,kutoka Morogoro,anatarajia kurelease albam yake mpya hivi karibuni baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu
Afande ambae alitamba na ngoma zake nzito kipindi cha nyuma zilizokuwepo kwenye album yake ya kwanza kabisa iliyokwenda kwa jina la Darubini Kali, yuko mbioni kuachia album yake mpya ambayo itakwenda kwa jina la ''Kingdom Ya Amani Na Upendo''.
Mpaka sasa rapper huyo hajasema album hiyo imebeba ngoma ngapi na ameshirikiana na wasanii gani na wangapi.
Endelea kutembelea blog yetu uburudanike zaidi.

video mpya ya Mabeste ft Deddy hii hapa.